Edward Ombui Swahili short story writer, poet and winner of Taifa Leo Annual Insha Competition

Mapenzi Takataka,na Edward Ombui

                       Nilipokuona

                       Zama nyaka thelathini

                       Ulifungua fuadi yangu

                       Kwa nyimbo zako

                       Nyimbo za mdundo wa kuvutia

                      Nikasisimka

                      Kwa sauti yako laini

                       Na huba zako shubiri

 

Siku ya ndoa

                          Tukaapa kuwa wamoja

                            Mbele ya waja leo

                          Karibu na vipaza sauti

                          Mirindimo ya ngoma ikiandamana

                           Kwa mahadhi na miondoko isiyo kifani

                          Tukaahidi kuvaa njuga

                          Ulimwengu kupambana

 

Baadaye

                      Ukageuka nusu kichaa

                    Ukatembea na viruka njia

                      Wendawazimu wasio timamu

                       Ukaniachia hisia

                       Hisia za majuto moyoni

                      Ukanipondaponda

                     Maungo yangu yakalegea

                     Ningajua!

 

Sasa

        Nasuhihi usiniangaishe

        Nenda zako tafadhali

         Enenda wendako

        Toka nenda usirudi

        Mimi si mwenzako tena

   Copyright © Edward Ombui,2019

________________________________________________________

Edward Ombui,is Swahili short story writer, poet and winner of Taifa Leo Annual Insha Competition. Edward who developed his reading culture at a tender age,loves reading novels and performing spoken word poetry.He has written several short stories and over 100  Swahili poems that are to be published soon. He adds that his works are based on themes such as tribalism, domestic violence, religious hypocrisy and bad governance.He has been featured in Kenyan Newspapers and won a creative writing competition among other achievements.

 

Advertisements

One thought on “Mapenzi Takataka,na Edward Ombui

 1. Edward Ombui Mogusu says:

  Bobea uwe kioo. Uwe mtu wa pekee, kurunzi ya pekee, kiongozi wa pekee na rafiki wa pekee. Elimu huhitaji watafiti wala si utafishi, Watafiti ndio wapatao ukweli wa mambo lakini watafishi huzua tafrani, tafashi na mtafaruku. katika elimu vitu hivyo havifai wala havitakikani kwani havitawafikisha watu katika kuelewa, kuerevuka wala kutaalamika kidedea. Waulize wajuao. wewe ni mja kama waja wengine, ukiujua huu, huu hauujui,kubali. Ungali una nafasi kubwa ya kujifundisha. Elimu ni bahari.

  wako,
  Edward Ombui
  Almaarufu
  Malenga Mdogo.
  2019

  Like

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s